Bondia Chris Eubank Jnr {pichani kulia} akimuangalia mpinzani wake Liam Smith baada ya kumpiga ngumi kali ya kidevu iliyompeleka chini na kufanya refa wa mchezo Kevin Parker kumuhesabia bondia Smith.Hata hivyo Chris Eubank alifanikiwa kumshinda mpinzani wake kwa ushindi wa TKO raundi ya 10 baada ya refa kusimamisha mchezo kwa kuona Liam Smith hamuwezi Chris Eubank Jnr. 


 Chris Eubank Jnr {kulia}akimsukumia makonde mazito Liam Smith na kumfanya ashindwe kuendelea na pambano kwenye raundi ya 10.Ikumbukwe hili ni pambano la marudiano pambano la kwanza Liam Smith alishinda kwa Tko na hili la pili Chris Eubank ameshinda kwa Tko.