Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro,Kasilda Mgeni ametoa onyo kali kwa Mwekezaji wa kampuni ya uwekezaji ya LM Investment inayozalisha Katani Wilayani hapo ambayo hivi karibuni imezua mjadala mkali mitandaoni uliozua taharuki kwa kuwashutumu wanakijiji wa kata ya Maore Wilayani hapo kuvamia eneo lake la uwekezaji kwa kukata na kuchoma mikonge yake.Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo wakati akizungumza na wanavijiji vitatu vya Mpirani,Msufini na Ndungu Jana Septemba 10 ambapo amemtaka mwekezaji huyo kuacha mara moja kusambaza mitandaoni taarifa za uongo zenye kuzua taharuki na zenye kuichonganisha serikali na Wananchi jambo linaloharibu taswira ya serikali ionekane kwamba haiwajali wawekezaji,kitu ambacho si cha kweli,bali kazi ya Serikali ni kuondoa kero,kulinda wawekezaji na kutetea wanyonge.
“Mimi nitumie Mkutano huu kumuonya muwekezaji juu ya vitendo vyake vya taharuki ya kudanganya watanzania kwamba Wananchi wa Ndungu,Msufini na Mpirani wanavamia maeneo yake na kuchoma mkonge,Nampa onyo atakaporudia tena serikali haitamwacha tutamchukulia hatua za kisheria kwasababu anaichonganisha serikali na wananchi” amesema Mgeni
Mgeni ameongeza kwa kuwataka wanakijiji wa kata ya Maore wawe na mahusiano mazuri na mwekezaji ili kuwepo na Maendeleo yenye tija kati ya mwekezaji na wanakijiiji huku akiwataka kuhakisha zoezi la malipo ya ankara ya umilikishwaji wa viwanja hekta 300 walizopewa na serikali ya Tanzania yanafanyika mapema.

0 Comments