Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), wameshauriwa kutoacha kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo (ARV's) ghafla, hata kama watapimwa na wataalam wa afya na kuonekana kuwa hawana tena virusi hivyo ili kujiepusha na madhara yatakayowapata.Waziri mkuu ametoa wito huo jana siku ya Alhamis ya tarehe 7 septemba 2023 jijini Dodoma kwenye mkutano mkuu wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Tanzania {NACOPHA}.
Waziri mkuu amesisitiza watuamiji wengi waliotumia dawa hizo kwa muda mrefu na waliporudi kupimwa na kukutwa hawana virusi tena waliacha dawa hizo kwa ghafla na baadae walipatwa na madhara.
0 Comments