Wanamgambo wa kijihadi wameshambulia boti kaskazini-mashariki mwa Mali, na kuua takriban raia 49, serikali ya mpito ilisema.
Pia waliripotiwa kushambulia kambi ya jeshi na kuua wanajeshi 15, huku wapiganaji wapatao 50 wakisemekana kufariki.
Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
Tishio la kushambuliwa na wanamgambo hao limekuwa likiongezeka licha ya madai ya jeshi kwamba mamluki wa Wagner wa Urusi wanageuza mkondo wa kampeni yao.
Mji wa kaskazini wa Timbuktu umekuwa chini ya vizuizi tangu mwisho wa mwezi uliopita na kumekuwa na mashambulizi mengine kadhaa ya hivi majuzi dhidi ya vyombo vya usafiri.
BBC haikufanikiwa kuthibitisha ripoti ya hivi punde ya serikali, ambayo ilisomwa kwenye TV ya kitaifa.
Wanamgambo wanaripotiwa kushambulia boti hiyo ilipokuwa ikisafiri kwenye Mto Niger kutoka mji wa Gao kuelekea Mopti.
Wanamgambo pia walishambulia kambi ya jeshi katika Mzingo wa Bourem katika eneo la Gao.
Jeshi la Mali lilisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba boti hiyo imeshambuliwa mwendo wa saa 1100 GMT na "makundi ya kigaidi yenye silaha".

0 Comments