Waungwana ndugu zangu Watanzania popote duniani mlipo pichani ni ndugu yetu anayejulikana kwa jina la Rashid Maganga maarufu kwa jina la Chidy,Amekuwa akiishi jijini Johannesburg kwa muda wa miaka 20 bila kurudi nyumbani hata mara moja na hana mawasiliano na ndugu zake nyumbani Tanzania.
Kabla ya kwenda South Africa alikuwa akiishi Kiwalani na baadae akahamia Tandika,ana dada yake anaitwa Lucy Maganga.
Ndugu yetu Rashid amepatwa na mtihani wa maradhi ya kupooza hivyo hawezi kuongea wala kutembea.
Tunachoomba ndugu,jamaa au marafiki wanaomfahamu ndugu yake yoyote kwa nyumbani Tanzania chondechonde tuwasiliane kwa namba hizi hapa.
+27 787 081 218
+27 781 688 121
Kwa umoja wetu ni matumaini yetu tutasaidiana kuitafuta familia ya ndugu yetu Rashid Maganga {Chidy}.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.

0 Comments