Kikosi cha Watanzania kutoka Ufaransa nacho kilishiriki mashindano hayo ya Serengeti Footballa Bonanza yaliyofanyika jijini Den Haag jana tarehe 09.09.2023 ambapo mshindi wa mashindano hayo ilikuwa ni timu ya Kilimanjaro kutoka Sweden.
Baadhi ya watu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali walishiriki kuja kushangilia timu zao
                                    Kikosi cha timu kutoka Ufaransa
                                      Kikosi cha Serengeti Fc kutoka Antwerpen Ubelgiji

Golikipa bora wa mashindano ya Serengeti Football Bonanza The Black Braa akiwa na kikombe chake na medali yake 
Msemaji wa timu kubwa barani Afrika Dar es Salaam Young Africans Hajji Manara mwenye kofia akiapata picha na baadhi ya watu na golikipa wa timu ya Serengeti kutoka Antwerpen Ubelgiji.
Golikipa bora wa mashidano na timu ya Serengeti kutoka Antwerpen Ubelgiji akipokea zawadi yake kama kumbukumbu ya mashindano ya Serengeti Football Bonanza yaliyofanyika jijini Den Haag tarehe 09.09.2023 na timu ya Kilimanjaro Ff kutoka Sweden walitwaa ubingwa wa mashindano hayo

Baadhi ya waratibu wa Serengeti Football Bonanza wakitoa maneno ya shukrani kwa wachezaji na waageni waalikwa waliofika  uwanjani hapo jana katika jiji la Den Haag nchini Uholanzi.
Pichani ni nahodha wa timu ya Serengeti ndugu Ronda akinyanyua kikombe juu cha kushangilia kwa kujinyakulia nafasi ya tatu katika mashindano ya Serengeti Football Bonanza yaliyofanyika jijini Den Haag nchini Uholanzi hapo jana tarehe 09.09.2023

Kikosi cha Leeds ya Uingereza ambacho jana kiliweza kufuzu mpaka fainal ila kwa bahati nzuri wakajaaliwa kuchukua nafasi ya pili.

Pichani kulia ni Ghanim kutoka Leeds ya Uingereza ambaye alikuwa mfungaji wa goli bora katika Bonanza hilo ambalo liloifanyika nchini Uholanzi siku ya tarehe 09.09.2023