Mo Salah
Al-Ittihad wako tayari kutoa dau la pauni milioni 200 kwa ajili ya mshambuliaji wa Liverpool kutoka Misri Mohamed Salah, 31, kabla ya dirisha la usajili la Ligi ya Saudia kufungwa tarehe 7 Septemba. (Mail)
Liverpool tayari ina mbadala wa Salah aliyepangwa na huenda wakamnunua winga wa PSV Eindhoven raia wa Ubelgiji Johan Bakayoko, 20, mwezi Januari ikiwa mshambuliaji huyo wa Misri ataamua kuondoka. (Express)
Mason Greenwood
Lazio iliamua kutomsajili mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Mason Greenwood mwenye umri wa miaka 21 kabla ya kujiunga na Getafe kwa mkopo siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho. (Goal)
Mazungumzo ya Atletico Madrid na Tottenham kumhusu kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28, yalimalizika baada ya Spurs kukataa ofa ya kwanza kwani haikujumuisha wajibu wa kununua. (Fabrizio Romano)
Che Adams ( katikati aliyevaa jezi namba 10)
Southampton ilizuia uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Uskochi Che Adams mwenye umri wa miaka 27 kwenda Wolves . (Athletic - subscription required)
Mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino anasema dirisha la usajili limekuwa "gumu" licha ya timu yake kutumia zaidi ya pauni milioni 360 msimu huu. (FourFourTwo)
Nicolas Pepe
Winga wa Ufaransa Nicolas Pepe, 28, anaweza kuondoka Arsenal na kuelekea Saudia ambayo haijatajwa jina lake kabla ya dirisha la usajili la Pro League kufungwa tarehe 7 Septemba. (Football London via Fabrice Hawkins)
Arsenal ilifikiria kusitisha kandarasi ya Pepe mnamo Ijumaa, mwaka mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wake, baada ya mpango wa kuhamia Besiktas kushindwa. (Mail)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anatarajiwa kumpanga kiungo wa kati wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 21 na mchezaji mpya Ryan Gravenberch katika nafasi ya namba nane katika safu ya kati. (Express)
Bayern Munich ilishindwa kulenga shabaha tatu katika siku ya mwisho ya uhamisho - kiungo wa Ureno Joao Palhinha, 28, alibakiwa na Fulham , mlinzi wa kati wa Ujerumani Armel Bella-Kotchap, 21, aliamua kuhamia kwa mkopo PSV Eindhoven kutoka Southampton na mlinzi wa Chelsea Muingereza Trevor Chalobah, 24, anaonekana kubakia Stamford Bridge. (Goal)
Pendekezo la Bournemouth la kutaka kumnunua mshambuliaji wa Leicester City na Zambia Patson Daka, 24, halikufaulu katika saa za mwisho za dirisha. (Goal)
Mlinzi wa Senegal Mamadou Fall, 20, alikamilisha uhamisho wa mkopo kutoka klabu ya MLS Los Angeles FC kwenda Barcelona siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho, akiwa na chaguo la kufanya uhamisho wa kudumu wa £5.6m
Winga wa Jamaica Demarai Gray, 27, atasalia Everton , licha ya ofa kutoka kwa klabu ya Saudi Arabia. (Sky Sports)






0 Comments