Waziri mpya wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki, na Naibu wake Mhe. Dunstan Kitandula leo Septemba 5,2023 wamepitishwa katika mikakati mbalimbali ya kisekta.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, ndiye aliyoiongoza  Menejimenti ya  Wizara kuwapitisha viongozi hao Wakuu waliokabidhiwa ofisi zao   Jana mtumba jijini  Dodoma.

Katika kikao hicho wakuu wote  wa Idara walihudhuria na kuwasilisha  Mawasiliano kadhaa.

 Akiwakaribisha viongozi hao katika kikao kazi hicho Dkt. Abbasi amefafanua kuwa Wizara hiyo inayochangia asilimia 21 ya Pato la Taifa na 25 ya Fedha za Kigeni ina mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato la muhimu ni uwekezaji zaidi katika uendelezaji na utangazaji wa utalii.

Mhe. Kairuki ameteuliwa katika  Wizara hii akitokea Wizara ya TAMISEMI wakati Mhe. Kitandula amekuwa Mbunge.