Ibada Maalum ya kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Moringe Sokoine, imefanyika leo April 12,2024 nyumbani kwake katika kijiji cha Enguik Monduli Juu,Wilayani Monduli Mkoani Arusha.


Aidha Ibada hiyo imehudhuriwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi wengine wa serikali na wageni kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi,

Akizungumza katika kumbukizi hiyo Leo Monduli Dkt. Samia amesema kwamba yapo mambo matatu ya kujifunza kwa Watanzania kwa Hayati Edward Moringe Sokoine ikiwemo suala la uwajibikaji Kupinga vita Uhujumu Uchumi, Ubadhilifu wa mali za Umma, pamoja na kusimamia maelekezo ya viongozi wakuu kwa vitendo.

"Kazi ndio njia pekee ya kulijenga Taifa lililo huru.. Bila kazi hatuwezi kuwa huru, 12februari 1983. Taifa lenye Afya na elimu ni Taifa lenye nguvu kisiasa na kiuchumi'
Dkt. Samia aliweza kutoa baadhi ya Nukuu za Hayati Edward Moringe Sokoine ya mwaka 1980/

Alisema viongozi wa serikali wanapaswa kuwajibika katika nafasi zao za uteuzi kwani uongozi ni dhamana ambayo wamekabidhiwa inayowataka siku zote kutekeleza kwa bidii kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na sio vinginevyo.

Aidha ametilia mkazo kwamba Hayati Sokoine alikuwa akisisitiza uwajibikaji kwa watendaji wa serikali ,mara zote enzi za uongozi wake alikazia suala la uadilifu katika utendaji na kupiga vita rushwa ,Uhujumu Uchumi na Ubadhilifu wa Mali za Umma hivyo ikiwa ndiyo njia pekee ya kumuenzi Sokoine, kwa viongozi ni kuwajibika kwa hilo ili wananchi waweze kuiamini serikali yao.

Akiongoza Ibada hiyo Mhashamu Askofu Isaac Amani Jimbo kuu katoliki Arusha alisema Alisema jambo lingine alilokuwa akisisitiza Sokoine ni suala la elimu kwani suala hilo lilikuwa kipaumbele chake kitaifa na aliwataka viongozi wa serikali kufanya hivyo kwa vitendo katika maeneo yao ya Kazi.

Mhashamu Amani lisema pamoja na kuhimiza Jamii ya kifugaji kupeleka watoto shule ye ye alikuwa kwao kama shujaa na w alikuwa wanajivunia ye ye kwani alipenda kutunza mazingira

Edward Moringe Sokoine anakumbukwa kama kiongozi Mzalendo, mchapa kazi alikuwa mtetezi wa usawa kwa wote, alichukia rushwa na Alicia Vita vijana kitumia dawa za kulevya kwani zonadhoogisha ngivu kazi za Taifa na jamii kwa ujumla.

Akitoa Salam za Familia Joseph Edward Sokoine amesema kuwa ni kweli kwamba baba yao aliwatoka ghafla miaka 40 iloyopita, japokuwa hayupo nao kimwili Ila ndani ya mioyo yao atadumu kwani kupita kwa miala hakuwezi kufuta kumbukimbu ya upendo wake kwao.

"Tunaendelea kukumbuka kwa mema ya pekee kila. Siku na tunamshukuru Mungu kwaajili ya mika iloyopita, Saudi ya itaendelea kusikika masikioni meeting, kicheko chako tabasamu, Lakota limebakia mioyo ni mwetu vikitufariji" Alisema Joseph Sokoine huku akiwa amegubikwa na Majonzi.

Hayati Edward Morninge Sokoine alizaliwa 1agosti 1938 katika Kijiji cha Monduli Juu wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha akiwa mototo wa Watatu kati ya watoto watano wa mzee Sokoine Sepere na Bibi Napelel Sokoine

Alipata elimu ya while ya msingi na sekondari kati ya make 1948-1958 ambapo mwaka 1960 alijiunga na chama cha TANU kilichopigania Uhuru, Alifanya masomo. Yake ya juu kwenue kilichokuwa chuo cha uongozi change Mzumbe na kisha aliendelea na magunzo zaidi nchini Ujerumani kwenue masuala ya uongozi na usimamizi wa fedha, aliporejea nchini aliteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wilaya ya Maasai (District Executive Officer -Maasai District) ambayo inakulikana kwa sasa kama wilaya ya Monduli.

Kwenye uchaguzi Mkuu wa wabungena Rais mwaka 1965 aligombea na kushinda ununge wa Jimbo la uchaguzi la Maasai mwaka 1967,aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa waziri mdogo wa Wizara ya Mawasiliano, baada ya uchaguzi Mkuu 1970 aliteuliwa kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na aliendelea kuwa na wadhifa huo hadi mwaka 1972