Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amirabdollahian amesema Iran itatoa jibu la haraka iwapo kutakuwa na shambulio kubwa kutoka kwa Israel.

Katika mahojiano na NBC News siku ya Ijumaa, Amirabdollahian alisema ikiwa Israel itachukua hatua kinyume na maslahi ya Iran, "jibu linalofuata la nchi yake litakuwa la haraka na litakuwa katika kiwango cha juu zaidi".

Amirabdollahian alipuuza shambulio linalodhaniwa kuwa la ndege zisizo na rubani za Israel dhidi ya Isfahan katikati mwa Iran, akihoji iwapo Israel ilihusika.

Alisema droni ndogo zilizoshambulia zilikuwa "kama wanasesere wanaotumiwa na watoto wetu kuchezea".