DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde leo April 4, 2024 amefanya ziara kukagua ujenzi wa uzio na ukarabati wa madarasa ya Shule ya Msingi Uhuru jijini Dodoma ambayo ni moja ya shule kongwe za jijini humo

Katika ziara hiyo ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa marekebisho makubwa ya miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo kwa shule nyingi za Dodoma Jiji ikiwemo Shule ya Msingi Uhuru.

“Serikali imeleta fedha hapa kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hii kongwe iliyojengwa mwaka 1928,kwa kuwa hali yake haikuwa ya kuridhisha ila kwa ukarabati huu itairudisha shule hii kongwe katika hali yake ya kawaida.

“Na mimi kama Mbunge wa eneo hili nimeona niunge mkono jitihada za serikali kwa kuanzisha ujenzi wa uzio wa shule hii kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na kuweka mazingira mazuri ya kusoma

Amesema kwa sasa eneo hilo lina muingiliano mkubwa sana wa wafanyabishara na watoa huduma mbalimbali ambao shughuli zao zinaathiri wanafunzi kusoma kwa utulivu.