MWENGE wa Uhuru Kitaifa unatarajiwa kukimbizwa wilayani Muheza Aprili 15 mwaka huu ukitokea wilaya ya Tanga na utazindua miradi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 4 ya maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah alisema kwamba maandalizi ya kupokea mwenge huo yanaendelea vizuri na utakapokuwa wilayani humo utakimbizwa umbali wa kilomita 84.

Alisema katika kilomita hizo Mwenge huo utapita kwenye tarafa 3 kata 9 kati ya 37na vijiji 18 kati ya 126 na vitongoji 35 kati ya 464 ambapo miradi 8 ya maendeleo itakaguliwa,kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi.

Mkuu huyo wa wulaya alisema kwamba katika miradi hiyo kutakuwa naya maboresho ya miundombinu ya majisafi na salama kitisa hadi Muheza uliopo Kata ya Genge utaka,Ujenzi wa daraja barabara ya Genge-Mangenya uliopo kata ya Genge.

Alisema pia miradi mengine ni Ujenzi wa muindombinu ya maji taka,vyoo matundu 5,zahanati ya Nkumba uliopo kata ya Nkumba,Mradi wa Kiwanda cha kusindika mazao ya viungo katika mfumo wa kilimo-hai GFP Organic LIMITED uliopo kata ya Nkumba,Ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa,ofisi za walimu 03,matundu 12ya vyoo vya wanafunzi.

Mkuu huyo wa wilaya alibainisha pia watakagua mradi wa jengo moja la utawala katika shule ya Sekondari Magila iliyopo kata ya Magila ,ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Magila,mradi wa uzoaji taka wa vijana kikundi cha wazo jipya kilichopo kata ya Genge.

“Lakini pia mbio hizi zitakagua mradi wa kitega uchumi ,Ujenzi wa Hotel iliyopo kata ya Majengo na utekelezaji wa kauli mbiu mradi wa mazingira chuo cha Tari-Mlingano “Alisema

Hata alisema kwamba Mwenge wa Uhuru utapokelewea katika Kijiji cha Mkanyageni uliopo wilayani Muheza ukitokea wilaya ya Tanga ambapo mkesha wake utafanyika kwenye uwanja wa Jitegemee utakaopambwa na wasanii 10 wa bongo fleva hapa nchini akiwemo Alikiba.

Na Oscar Assenga,MUHEZA.