Iran ni kubwa zaidi kuliko Israel kijiografia na ina idadi ya watu karibu milioni 90, karibu mara 10 zaidi ya Israeli - lakini hii haimaanishi kuwa ina nguvu kubwa zaidi ya kijeshi.

Iran imewekeza fedha nyingi kwenye makombora na ndege zisizo na rubani. Ina hifadhi kubwa ya silaha hizo lakini pia imekuwa ikitoa kiasi kikubwa kwa washirika wake - Wahouthi nchini Yemen na Hezbollah nchini Lebanon.

Inachokosa ni mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga na ndege za kivita. Urusi inaaminika kushirikiana na Iran kuboresha hizo, kwa kurudisha msaada wa kijeshi ambao Tehran imetoa Moscow katika vita vyake na Ukraine - hasa katika mfumo wa ndege zisizo na rubani za Shahed ambazo Warusi sasa wanaripotiwa kutengeneza wenyewe.

Kwa upande wake, Israeli ina moja ya vikosi vya anga vya juu zaidi ulimwenguni. Kulingana na ulinganishi wa kijeshi wa IISS, Israel ina takriban vikosi 14 vya ndege - ikiwa ni pamoja na F15, F16 na ndege za hivi punde za F-35.

Israel pia ina tajriba ya kufanya mashambulizi ndani kabisa ya maeneo ya mahasimu wake