KATIBU wa Itikadi Uenezi na Mafunzo CPA Amoss Makala amewakikishia wananchi wa Mbagala kuwa mabasi ya mwendo kasi yataanza kutoa huduma kuanzia Desemba mwaka.huu.


Kauli hiyo ya CPA Makala imeacha faraja kwa wakazi wa Mbagala ambao wamekuwa wakisubiria kuona mabasi ya mwndo Kasi yalianza kutoa huduma baada ya ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi hayo kukamilika kwa asilimia kubwa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku 10 katika Mkoa wa Dar es Salaam,CPA Makala ambaye pia ni Mlezi wa Mkoa huo kichama amesema tayari Chama kimefanya mazungumzo na Serikali kuhusu mradi huo ,hivyo uhakika mradi wa mabasi ya mwendo Kasi utaanza Desemba mwaka huu.

Amesema mabasi ya mwendo Kasi 200 ya kuanzia yanahitajika kwa ajili ya kutoa huduma,hivyo ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuwa watulivu na kusisitiza miundombbinu ya barabara ya mradi ilishakamilika muda mrefu na kilichobakia ni kuanza kwa huduma tu.

CPA Makala ambaye amehitimisha ziara yake Mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Uwanja wa Maturubai wilayani Temeke amesema pamoja na kukagua miradi ya maendeleo lakini habari njema kwa wananchi hao ni kuhusu mradi huo.

Pamoja na hayo amezungumzia changamoto ya vibanda katika pembezoni mwa barabara ya mwendo kasi na hivyo ametoa maelekezo kwa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads)na TAMISEMI kukaa meza ya mazungumzo kupata ufumbuzi mapema huku akisisitiza lazima barabara hiyo ichangamke watu wafanyabiashara.

Kwa upande wa viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa huo Abbas Mtemvu ameeleza kuwa ziara ya CPA Makala katika majimbo ya 10 imeacha hamasa kubwa ndani ya Chama na wananchi kwa ujumla.