Mahakama kuu ya India imesema ubakaji na mauaji ya hivi majuzi ya daktari tarajali katika jimbo la Bengal Magharibi "umeshtua taifa" na kukosoa mamlaka kwa jinsi walivyoshughulikia uchunguzi.

Mwili wa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 ulipatikana mapema mwezi huu katika chumba cha semina cha hospitali ya serikali huko Kolkata alikofanyia kazi.

Mfanyakazi wa kujitolea wa hospitali amekamatwa kuhusiana na uhalifu huo, na Ofisi Kuu ya Upelelezi sasa inachunguza kesi hiyo.

Uhalifu huo umesababisha maandamano makubwa nchini humo.