UJERUMANI : Shirikisho ya Kupambana na Uhalifu nchini Ujerumani, BKA, imesema idadi ya watu wanaoshukiwa kuhamia Ujerumani kinyume cha sheria imeongezeka kwa kiasi kikubwa mwaka 2023.

BKA imedai kuwa idadi ya wahamiaji haramu imefikia 266,224 ambao wameingia na kuishi bila kibali mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 33.4, ikilinganishwa na mwaka 2022.

SOMA: Wahamiaji haramu wakamatwa shamba la michungwa

Kwa mujibu wa Shirika la Ulinzi wa Mipaka ya Ulaya imesema takribani watu 380,200 waliovuka mipaka bila idhini kwenye eneo la Schengen