Mwanamasumbwi Jake Paul aliacha doa la kudumu kwenye urithi wa ndondi wa bingwa mara mbili wa uzito wa juu Mike Tyson kwa kushinda kupitia uamuzi wa pamoja mbele ya mashabiki 70,000 Texas - na kufuatiliwa na mamilioni ya watu waliotazama pambano hilo kupitia Netflix.
Jake Paul na Mike Tyson walikwenda raundi zote nane, huku Paul akiibuka mshindi kupitia uamuzi wa pamoja.
Mara tu baada ya pambano hilo, Paul alikuwa mnyenyekevu kuhusu ushindi wake, akisema, "Kwanza kabisa, Mike Tyson ... ni heshima kubwa. Mike, yeye ni mkongwe, nimetiwa moyo naye, na tusingekuwa hapa leo bila yeye.”
Tyson alizungumza juu ya uchezaji wake, akisema, "Sikuthibitisha chochote kwa mtu yeyote, ila mimi mwenyewe."
Pia alitoa kongole kwa Paul kama mwanariadha, akisema, "Yeye ni mpiganaji mzuri sana."
Mike Tyson sasa ameshindwa mara saba kwenye rekodi yake ya kitaaluma.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 58, anayeshindana kwa mara ya 59, amepoteza mapambano yake matatu ya mwisho, ingawa mara ya mwisho alipanda ulingoni katika nafasi ya kitaaluma kabla ya usiku wa leo ilikuwa mwaka 2005.
Kwa upande wa Paul huu ni ushindi wa 11 Kati ya mashindano 12 aliyowahi kufanya.
0 Comments