DAR ES SALAAM; DAR ES SALAAM; ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, amesema ni vyema Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akapumzika na kumuachia uenyekiti Tundu Lissu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Lema amesema Mbowe ameifanyia makubwa Chadema, lakini umefika wakati sasa akapumzika na jukumu hilo likabaki kwa Lissu ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.

Freeman Mbowe“Mwenyekiti familia zetu zinafahamiana ni ndugu yangu, sio adui yangu, lakini leo nimekuja kumuomba apumzike amuachie Lissu kazi ya uenyekiti, apumzike. Tuanavyosema Mwenyekiti apumzike hatuna maana hana nguvu,” amesema Lema ambaye pia amepata kuwa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chadema.

TUNDU LISSU

Mbowe na Lissu wote wamechukua  fomu kuwania nafasi ya uenyekiti wa Chadema katika uchaguzi utakaofanyika Januari 21, mwaka huu.