RAIS Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika tamasha la uimbaji na maombi ya kuombea Uchanguzi Mkuu lililoandaliwa na Kwaya ya Zabron Singers linatarajia kufanyika Aprili 13, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City.

Akizungumza na habari leo Katibu wa Zabron Singers Emmanuel Zabron amesema tamasha hilo linalojulikana kama ‘Mkono wa Bwana Bessing’ linatarajia kutoa fursa kwa waimbaji wachanga wa nyimbo za injili kumsifu Mungu na kuombea Taifa kuelekea uchaguzi.

“Tunapokaribia kipindi muhimu kwa taifa letu, kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais na wabunge tuna waalika waumini wote kushirikaina nasi katika tukio hili la jamii kwa ajili ya kuombea Taifa.

“Lakini pia kupitia tamasha hili ni sehemu ya kuendeleza vipaji vya vijana wa Afrika Mashariki, ili wawe na ushawishi mkubwa katika muziki na maisha yao ya kiroho katika kumtumikia Mungu,”amesema Emmanuel Zabron,

Aidha Emma amesema fedha zinazopatikana katika tamasha hili zitatumika kuanzisha kituo cha huduma za jamii ili kuhamasisha kipawa chao cha injili katika kutangaza neno la Mungu.