Kuanzia kushoto, mchezaji wa Morocco, Achraf Hakimi, wa Misri, Mohamed Salah na wa Cameroon, Andre Onana - timu zao ni vinara wa makundi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 kuelekea raundi ya tano.
Mechi za Mataifa ya Afrika za kufuzu Kombe la Dunia la Fifa 2026 zinaendelea tena wiki hii baada ya kusimama kwa miezi tisa.
Baadhi ya mechi zilizoanza Alhamisi na Ijumaa zimeshuhudia DRC ikiifunga 1-0 Sudan Kusini, Rwanda ikalala nyumbani 0-2 dhdi ya Nigeria, Afrika Kusini ikaibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Lesotho, Kenya ikaenda sare na 3-3 ugenini na Gambia na Ghana ikiirarua 5-0 Chad.
Tanzania itakipiga na Morocco ugenini siku ya Jumatano.
Timu sita katika kila kundi, hucheza mechi 10, na mechi mbili zitachezwa mwezi huu na zitasaidia kuamua hatima ya timu nyingi. Washindi tisa katika makundi wanakata tiketi ya kucheza kombe hilo nchini Canada, Mexico na Marekani.
DR Congo
Mabadiliko ya usimamizi yametokea tangu duru iliyopita mwezi Juni, huku Nigeria, Senegal na Tunisia zikiwa miongoni mwa timu zilizo na makocha wapya.
0 Comments