MAHAKAMA ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara imemhukumu kifungo cha maisha jela Hassan Hakika ,18, baada ya kumpata na hatia ya kumlawiti mtoto mwenye ulemavu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleiman amesema mfungwa huyo alimlaghai mtoto huyo na kisha kwenda naye kichakani ambako alimfanyia ukatili huo.

SOMA ZAIDI: Ofisa mipango adaiwa kubaka mtoto kwenye gari

Kamanda Suleiman amesema mtuhumiwa alitenda tukio hilo mwezi Aprili 2025, katika kijiji cha Dinyeke mkoani Mtwara.

Katika hatua nyingine Mahakama ya Wilaya ya Masasi imewahukumu kwenda jela miaka 30 watu watatu baada ya kupatikana na hatia ya kulawiti katika matukio tofauti.

Watu hao ni Yujini Cleophane Venanti ,56, ambaye alilawiti mwanaume mwenye umri wa miaka ,28, mwingine ni Bakari Khamisi Matole ,21, ambaye alilawiti mwanafunzi wa kidato nne, ,17, na Danfrod Boniphance ,32, ambaye alimbaka mwanamke mwenye miaka 42.