Treni za mwendo kasi za Shinkansen za Japan kwenye njia yenye shughuli nyingi zaidi kati ya Tokyo na Osaka zilisimamishwa kwa muda baada ya nyoka kujilingalinga na nyaya za umeme.
Nyoka ya urefu wa mita alisababisha hitilafu ya umeme. Inasemekana alitambaa kwenye nguzo ya umeme na kufa alipokuwa akijaribu kutambaa kwenye waya zenye umeme mwingi.
Abiria mmoja alisema treni ziliendelea kuwa na umeme, zikiwemo taa na viyoyozi, lakini hazikufanya kazi. Huduma zilirejeshwa baada ya saa mbili.
Shinkansen ni mtandao wa reli ya mwendo kasi ambayo Japan ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuzindua huduma ya treni ya aina hii.
0 Comments