Gari lateketea wakati wa moto wa nyikani huko Meda, Ureno, Agosti 15, 2025.

Mwaka huu unatazamiwa kuwa wa pili au wa tatu kwa joto kali zaidi duniani katika rekodi, kuna uwezekano wa kuzidiwa na joto lililovunja rekodi la 2024, limesema Shirika la Umoja wa Ulaya la Copernicus Climate Change Service (C3S) siku ya Jumanne.

Ni taarifa ya hivi punde kutoka C3S baada ya mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa COP30 wa mwezi uliopita, ambapo serikali zilishindwa kukubaliana na hatua mpya za kupunguza utoaji wa gesi chafu, huku Marekani ikirejesha nyuma juhudi zake, na baadhi ya nchi zinataka kudhoofisha hatua za kupunguza CO2.

Hali mbaya ya hewa inaendelea kukumba nchi zote ulimwenguni mwaka huu. Kimbunga cha Kalmaegi kiliua zaidi ya watu 200 nchini Ufilipino mwezi uliopita. Uhispania ilikumbwa na moto mbaya zaidi wa mwituni kwa miongo mitatu kwa sababu ya hali ya hewa ambayo wanasayansi walithibitisha inatokana zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.

Mwaka jana ulikuwa ndio mwaka wa joto kali zaidi duniani katika rekodi.

Ingawa hali ya hali ya hewa ya asili hubadilikabadilika mwaka hadi mwaka, lakini wanasayansi wanasema ongezeko la joto duniani kunathibitisha kwamba sababu kuu ya ongezeko hili la joto ni utoaji wa gesi chafu kutokana na uchomaji wa nishati ya mafuta.

Miaka 10 iliyopita imekuwa miaka 10 ya joto zaidi tangu rekodi zianze kuhifadhiwa, Shirika la Hali ya Hewa Duniani lilisema mapema mwaka huu.

Kiwango cha kimataifa cha nyuzi joto 1.5 ni kikomo cha hali joto ambacho nchi ziliapa kisivuke chini ya makubaliano ya hali ya hewa ya Paris ya 2015, ili kuepusha matokeo mabaya zaidi ya ongezeko la joto.

Ulimwengu bado haujafikia lengo hilo – kwani wastani wa halijoto kimataifa ni 1.5 Selsiasi kwa miongo kadhaa.

Lakini Umoja wa Mataifa ulisema mwaka huu kwamba lengo la kupunguza Selsiasi 1.5 haliwezi kufikiwa kiuhalisi na kuzitaka serikali kupunguza utoaji wa hewa chafu ya CO2 haraka, ili kupunguza joto kuongezeka.