Frédéric Péchier, 53, daktari aliyewatilia sumu wagonjwa 30 kwa makusudi amehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Wagonjwa 12 kati yao 30 walifariki.

Péchier alibainika kuwawekea wagonjwa hao kemikali kama vile potassium chloride au adrenaline katika mojawapo ya matukio makubwa zaidi ya ukiukwaji wa matibabu nchini Ufaransa

Hukumu ya kesi dhidi yake ambyo ilidumu kwa miezi minne ilitolewa Ijumaa katika mji wa mashariki wa Besançon.

Mwathiriwa aliyekuwa na umri mdogo zaidi, mtoto wa umri wa miaka minne, alinusurika kupatwa na mshutuko wa moyo mara mbili wakati wa upasuaji wa kutoa uvimbe mdogo kooni mwake mwaka 2016.

Mwathiriwa aliyekuwa na umri mkubwa zaidi alikuwa na miaka 89.

"Wewe ni Daktari muuaji. Umedhalilisha madaktari wote," waendesha mashtaka walisema wiki iliyopita. "Umegeuza zahanati hii kuwa kaburi," walisema.