
WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amefanya kikao cha kazi na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, Naibu Waziri, Wanu Hafidh Ameir, pamoja na Timu ya Wataalam kutoka Wizara hiyo.

Kikao hicho ambacho kimefanyika jijini Dodoma pamoja na mambo mengine wamejadili mikakati mbalimbali yenye lengo la kendeleza sekta ya elimu nchini.

Katika kikao hicho pia, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo ameshiriki.
0 Comments