Mtu mmoja amewaua watoto wake saba pamoja na mtoto mwingine ambaye si wa familia hiyo katika tukio la mauaji ya risasi yaliyotokea Shreveport katika jimbo la Louisiana nchini Marekani, ambalo polisi wameelezea tukio hilo kama “mzozo wa kifamilia”.

Watoto hao walikuwa na umri wa kati ya mwaka 1 hadi miaka 14, kwa mujibu na shirika la habari la CBS ambalo ni mshirika wa BBC nchini Marekani.

Maafisa walisema tukio la risasi lilianza karibu saa 05:00 asubuhi (10:00 GMT) siku ya Jumapili. Mshukiwa alipiga risasi watu 10 kabla ya kukimbia kwa kutumia gari lililoibiwa, alisema msemaji wa Polisi wa Shreveport, Chris Bordelon. Polisi walimfukuza na hatimaye kumuua.

Wanawake wawili watu wazima, wakiwemo mama wa watoto hao, wako katika hali mahututi hospitalini.

Mshukiwa ametambuliwa kama Shamar Elkins, kulingana na mkurugenzi wa mawasiliano wa meya wa Shreveport, Leigh Anne Evensky, alivyoiambia BBC.

Inaripotiwa kuwa mshukiwa alimpiga risasi mwanamke mmoja barabarani kabla ya kwenda kwenye nyumba ya karibu ambako aliwaua watoto wanane, “mmoja kati yao hakuwa wa kwake”, polisi walisema.

Mtoto mmoja alifanikiwa kukimbia na kwenda kwenye nyumba ya jirani na kupiga simu polisi. Pia polisi walisema mshambuliaji alifanya tukio hilo peke yake. Mtoto aliyetoroka wa tisa aliruka kutoka juu ya paa na alikimbizwa hospitalini kwa matibabu, alisema Bordelon.

Akizungumza mapema Jumapili, Meya wa Shreveport Tom Arceneaux alisema: “Hili ni tukio la kusikitisha, pengine ni tukio baya zaidi la kusikitisha ambalo tumewahi kulipata Shreveport.