Vijana wapatao kumi kutoka baadhi ya mikoa mbali mbali wamefanikiwa kutinga katika kinyang'anyiro cha shindano la Vijana uchumi Challenge kwa mwaka wa 2026 ambalo kilele chake kinatarajiwa kufanyika Julai 6 mwaka huu katika ukumbi Mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Jenifa Omolo ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa halfa ya kufunga kambi rasmi ya vijana wapatao 100 ambao walikuwa wameweka kambi ya siku nne katika shule yaa uongozi wa Mwalimu Julias Nyerere iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani.
Katibu Oomolo amesema kwamba kambi hiyo ilikuwa na vijana wapatao 100 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania bara na visiwani ambapo wameweza kufanyiwa usahili na kufanyiwa mchujo kutoka kwa majaji mahiri wapatao saba ambaao waliweza kuzingatia vigezo mbali mbali katika kufanya maamuzi na kuangalia mawazo ambayo yaliwasilishwa na vijana hao.
"Nimefaarijika sana kuwa mgeni rasmi katika kufunga kambi hii rasmi ya vijana wapatao 100 na wametoka sehemu mbali mbali na vijana hao wameweza kufanyiwa mchujo naa kubakia vijana 100 kati ya 100 ambao walikuwa kambi na kwamba watakwenda sasa katika fainali ambayo itafanyika katika ukumbi Mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), jijini Dar es Salaam,"amebaisha Omolo.
Kadhalika ameongeza kwamba mshindi wa kwanza katika shindano hilo la Vijana Uchumi Challenge atajinyakulia kitita cha kiasi cha shilingi milioni 50, ambapo mshindi wa pili atajisshindia shilingi elfu 30 na mshindi wa tatu anaondoka naa kiasi cha shilingi milioni 20 huku washindi wengine watapata kifuta jasho.
Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuwapa sapoti kubwa na ushirikiano katika kuwawezesha vijana wote 100 waliofika hatua ya kambi ili kuhakikisha mawazo yao yanageuzwa kuwa miradi yenye tija.
Alifafanua Vijana Uchumi Challenge si shindano pekee, bali ni jukwaa la kuibua fikra za vijana, kulea ubunifu, kujenga ujasiri na kuthibitisha kuwa vijana wana nafasi kubwa ya kubuni suluhisho za changamoto za kiuchumi.
Omolo alibainisha kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Tanzania Bara ina vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 wapatao milioni 20.6, sawa na asilimia 34.4 idadi inayoonesha kuwa taifa lina nguvu kazi kubwa ambayo ikitumia vipaji na kuendelezwa ipasavyo inaweza kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi.
Aliwataka vijana kutumia simu janja kama nyenzo ya kujiongezea kipato kwa kutumia teknolojia, pamoja na kunufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na fursa nyingine zinazotolewa na Serikali.
Pia ametaja fursa nyingine kuwa ni mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kupitia mapato ya ndani, asilimia 30 ya zabuni zinazotengwa kwa makundi maalumu kupitia sheria ya manunuzi ya umma, pamoja na fursa zilizopo katika sekta za viwanda, uzalishaji na mnyororo wa thamani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Vijana Uchumi Challenge, Joseph Malekela, alieleza mashindano hayo yalizinduliwa Aprili 10, 2026, na baada ya kupokea na kuchambua maombi 7,852, vijana 100 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, walichaguliwa kuingia kambini.
Akisoma risala kwa niaba ya washiriki, Raiyan Juma Amour kutoka Zanzibar aliiomba Serikali kufanya tathmini ya kimkakati ya mawazo yote 100 yaliyowasilishwa ili yaweze kutumika katika sekta mbalimbali na kuchangia kuleta mageuzi ya kiuchumi na kutatua changamoto zinazoikabili nchi.
Katika kilele cha fainali za shindano hilo la Vijana Uchumi challenge kwa mwaka 2026 ambalo linatarajiwa kufanyika Julai 6 mwaka katika ukumbi Mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

.jpeg)
.jpeg)

0 Comments