
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize, amefunguka kuhusu uhusiano wake na Kajala Masanja, akisema kwa sasa wawili hao hawapo pamoja na wamefikia takribani miezi mitatu tangu kutengana.
Harmonize ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha jioni cha “31”, ambapo aliulizwa na Frida Amani kuhusu album yake mpya na kama ina wimbo wowote unaohusiana na Kajala, pamoja na hali ya uhusiano wao kwa sasa.
Akijibu, Harmonize amesema kwa sasa hayuko kwenye uhusiano na Kajala, huku akieleza kuwa suala hilo si jambo analoliona la kujivunia kiasi cha kulifanya kuwa stori ya kuendelea kuzungumziwa.
Amesema aliamua kukaa kimya kuhusu suala hilo kwa sababu anaamini si jambo jema kuendelea kulizungumzia hadharani, akisisitiza kuwa kwa sasa hakuna hisia za kimapenzi kati yao.

Hata hivyo, Harmonize amekataa kumzungumzia Kajala kwa undani, akisema kuwa yeye ni mtu mzuri.
“Maisha ogopa kumpa mtu kasoro”
Katika mazungumzo hayo, Harmonize pia amezungumzia upande wa maisha na mahusiano, akitoa kauli inayosisitiza umuhimu wa mtu kutowalaumu wengine kwa mapungufu ambayo yanaweza kuwa yanatokana na yeye mwenyewe.
Ametoa mfano wa Bi Mwendo, mhusika anayejulikana kupitia maigizo, akieleza kuwa hataki kuwapa watu wengine lawama kwa changamoto au mapungufu yanayoweza kujitokeza katika mahusiano.
Kwa upande wa uhusiano wake na Kajala, Harmonize amesema sababu ya yeye kuwa pamoja naye inapaswa kuangaliwa pia kutoka kwake mwenyewe, akieleza kuwa huenda amebadilika kitabia.
Amesema kwa sasa anajiona akifanya mambo tofauti na alivyokuwa mwanzoni, jambo ambalo linaweza kuwa sehemu ya sababu zilizochangia mabadiliko katika uhusiano wao.
Kauli hiyo ya Harmonize imekuja wakati mashabiki wakiendelea kufuatilia kwa karibu maisha yake binafsi, hususan uhusiano wake wa muda mrefu na Kajala.
0 Comments