Kwa ushahidi huu ni wazi kuwa mshtakiwa amesambaza nia yake kwa umma ya kuitishia serikali waheshimiwa majaji tukianza na mashahidi ambao walikuwa washtakiwa kisha baadaye wakaja kuwa mashahidi kifungu cha 151 cha sheria ya ushahidi urekebu wa 2023 kinasema kama hawa mashahidi walikuwa wamechochewa na maneno ya mshtakiwa ni washtakiwa wenza, lakini walikuwa na interest to serve na kwa mujibu wa kifungu hiki hawa ni mashahidi na wako compitent kutoa ushahidi.
Lakini sio tu kuishia kuwa wana interest to serve, je waliona video hawakuona walichocheka hawakuchochewa uzito wake ni kutokana na kile wanachosema na ili kuwadiscredit lazima ku prove wapi walisema uongo.
Waheshimiwa majaji hoja ya mwisho kabisa ilikuwa ni lalamiko kuhusu malalamiko ya ushahidi wa polisi, statement na ushahidi uliotolewa mahakamani.
Hayo sio contradiction bali ni futher elaboration of the witness. Haya si maneno yangu waheshimiwa.
Mahakama katika kesi ya Abeli Orua alias Matiku dhidi ya Jamuhuri criminial appeal number 421 ilieleza PW4 alitoa ufafanuzi zaidi mahakamani kuelezea zaidi kile alichofikisha kama maelezo polisi na hakukuwa na mpishano wowote.
Waheshimiwa majaji kwa kusema hayo submission yetu ndio hiyo kwa ushahidi wa mashahidi 17 ikiungwa mkono na ushahidi wa mashahidi wa utetezi hivyo tumefanya kazi yetu kwa ukamilifu na ni ombi letu mshtakiwa ahukumiwe sawasawa na shtaka lake.
Nasi tuwashukuru sana kwa kipindi chote mlichotusikiliza,kuanzia mwezi Septemba mwaka jana hadi mwaka huu mwezi Septemba mwishoni.
Tunashukuru kwa uvumilivu wenu.
Pia tunaomba kumshukuru kaka yetu japo hataki kwa kipindi chote ambacho tumekuwa naye kwenye kesi hii, kwa niaba ya Jamhuri hatukua na nia tofauti zaidi ya kuthibisha shtaka kwa kifungu hiki ambacho ni kwa mara ya kwanza kinakuwa tested.
Jaji: Shtaka limekuwa refu na haya yote lazima tuyasome na tutafakari tunawashukuru pia na wanachi walikuwa wanakuja wakati wote.
Kwa leo tunaishia hapa ushahidi ni mrefu tutahitaji muda wa kutosha ili tuweze kutoa maamuzi sababu hili ni shauri la namna yake, tutatoa hukumu tarehe sita mwezi wa kumi na moja saa tatu asubuhi.
0 Comments