Vikosi vya jeshi la Iran viko tayari kukabiliana na mashambulizi yoyote mapya ya Marekani, msemaji wa jeshi la taifa hilo Mohammad Akraminia amesema mapema hii leo.
Kauli hiyo imekuja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema amekataa pendekezo la Iran la kufungua tena Mlango bahari wa Hormuz na kusitisha mapigano.
Akraminia amesema vikosi vya Iran vimejiandaa kikamilifu kwa makabiliano yoyote, na kuonya kwamba Marekani itapata hasara kubwa iwapo itaanzisha shambulizi jingine dhidi ya Iran.
Awali, gazeti la Wall Street Journal liliripoti, likinukuu maafisa wa Marekani ambao hawakutajwa majina, kwamba Trump ataanzisha tena mashambulizi ya anga nchini Iran, baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula nchini Marekani kutamatika.
0 Comments