Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeahirishwa leo, Septemba 25, 2026, hadi Jumatatu, Septemba 28, 2026.

Kesi hiyo itaendelea kwa usikilizwaji wa uwasilishaji wa hoja za mwisho (Final Submission) kutoka kwa mshtakiwa.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Dunstan Ndunguru, anayeongoza Jopo la Majaji watatu linalosikiliza kesi hiyo.

Kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Lissu alikuwa akiendelea kuwasilisha hoja zake tisa za mwisho. Hadi muda wa kuahirishwa, alikuwa amefikia hoja ya saba inayohusu swali la “kama Jamhuri ya Muungano ilitishika” kutokana na maneno yaliyotumika katika mashtaka yanayomkabili.

Lissu aliomba muda wa mapumziko baada ya kufika saa saba kamili mchana, kama ilivyokuwa katika siku nyingine za usikilizwaji wa hoja hizo. Baada ya ombi hilo, jopo la majaji lilitoa uamuzi wa kuahirisha kesi hadi Jumatatu.