Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo Septemba 15, 2026, ameungana na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika Sala ya Jeneza ya Marehemu Bi. Maryam Shaaban Ramadhan, mama mzazi wa Katibu wa NEC, Idara ya Uchumi na Fedha ya CCM Taifa, Ndg. Jamal Kassim Ali.
Sala hiyo imefanyika katika Masjid Noor Muhammad, Kwa Mchina Mwanzo, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, ambapo Rais Dkt. Mwinyi amejumuika na ndugu, jamaa na wananchi kumuombea Marehemu kabla ya mazishi.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametoa pole kwa familia ya Marehemu, hususan Ndg. Jamal Kassim Ali, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo, huku akiwataka kuwa na subira na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.


.jpeg)


.jpeg)


.jpeg)


0 Comments