Mkazi wa Bunju A, LAURENCE Kweka (48), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, akikabiliwa na shtaka la kumuua mke wake Jane Urassa.
Kweka amefikishwa mahakamani hapo leo Oktoba 15, 2026 na kusomewa shtaka hilo linalomlabili na Wakili wa Serikali, Harrison Lukos, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kemilembe Josiah.
Inadaiwa Oktoba Mosi mwaka huu, huko Bunju A ndani ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua mkewe Jane Urrasa.
kabla ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa alielezwa kuwa haruhusiwi kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa shauri hilo halijafikia katika hatua ya kusikilizwa kwa ushahidi.
Hakimu Josiah alimweleza mshtakiwa kuwa kosa la mauaji linalomkabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, mahakama ilimweleza kuwa haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo la mauaji, hivyo mshtakiwa ataendelea kusalia mahabusu wakati upelelezi ukiendelea, kabla ya shauri hilo kupelekwa Mahakama Kuu kwa hatua zaidi.
Mahakama pia imeeleza kuwa shauri hilo litaendeshwa kwa njia ya mtandao wakati mshtakiwa akiwa mahabus. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 29, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa tena.

0 Comments