Na Oscar Assenga,TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga amezindua zoezi la Msaragambo Maalumu wa kila Mwei katika Mkoa huo maarufu Balozi Dk. Batilda Mazingira Day,unaolenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika usafi na utunzaji wa mazingira kuanzia ngazi za Mitaa na Vijiji huku watakaobainika kutupa taka ovyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumza mara baada ya kushiriki kufanya usafi,Dkt Batilda alisema kwamba wameunda kikosi kazi maalumu cha vijana 50 kitakachohusika na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira, kubaini maeneo yenye changamoto ya uchafu na kuchukua hatua kwa watakaobainika kutupa taka ovyo.

Kikosi hicho pia kitatekeleza sheria ndogo za mazingira zilizopo chini ya Halmashauri, ambapo watakaokiuka sheria hizo watakabiliwa na faini ya kuanzia Sh50,000.
Alisema kwamba kikosi hicho kitakuwa na jukumu la kukusanya taarifa na kubaini maeneo yanayohitaji usafi, kisha taarifa hizo kuwasilishwa kwenye Halmashauri husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua, ikiwamo kupeleka magari ya kuzolea taka.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba watakuwa na kamati ya ukaguzi itakayohusika na kubaini changamoto, kutoa elimu na maelekezo yatatolewa na pale sheria itakapokiukwa na wahusika wakionekana kuendelea kukaidi hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa miongozo.

"Niwaambie kwamba lazima tuhakikishe tunatunza mazingira na usafi ili baadaye tusije tukalaumiana na faini imeandikwa kwenye sheria ndogo za mazingira na Halmashauri faini ya chini ni Sh50,000," Alisema"Alisema RC huyo
Alisema kikosi hicho kimekaguliwa na kutambuliwa rasmi na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambalo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga litatoa ithibati na ruksa kwa kikosi hicho kushughulikia watakaokiuka sheria za mazingira.
Dk. Burian alisema faini zitakazokusanywa zitaingizwa katika mfumo rasmi wa ukusanyaji mapato, huku akisisitiza kuwa kikosi hicho hakitaruhusiwa kutumia nguvu wala kupokea rushwa wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.

"Timu hii haitakuwa juu ya sheria, watakula kiapo, hawatapokea rushwa wala kutumia nguvu kukamata na tozo zote zitakazokusanywa kisheria kupitia POS-Mashine na risiti zitatolewa. Tunataka kuhakikisha kwamba kosa linathibitishwa na hatua zinachukuliwa lakini tambueni kwamba hatukusudii kutoza faini kwa wananchi, tunakusudia kuboresha mazingira yetu," alisema.

Aliwataka wananchi kushiriki kwa hiari katika zoezi hilo, huku akizitaka Halmashauri zote 11 zilizopo mkoani Tanga, chini ya usimamizi wa Wakuu wa Wilaya, kuhakikisha zinatekeleza Msaragambo huo ambao umepewa jina la Balozi Dk. Batilda Mazingira Day, ukiwa na kaulimbiu maalumu ya utunzaji wa mazingira.
Dk. Burian alisema Mkoa wa Tanga unachangia Sh bilioni sita kwa mwezi katika pato la Taifa na kushika nafasi ya sita kati ya mikoa yote nchini, akisisitiza kuwa mafanikio hayo yanapaswa kwenda sambamba na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kuanzia ngazi ya kaya.

Akimwakilisha Mkurugenzi wa NEMC Kanda ya Kaskazini, Meneja wa NEMC Kanda ya Bagamoyo, Ndimbumi Mboneke, alisema kisheria kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha mazingira yanayomzunguka yanakuwa safi na salama wakati wote.
Alisema wananchi pia wana wajibu wa kutoa taarifa katika mamlaka husika pale wanapoona uharibifu wa mazingira.
"Sheria ya mazingira imetoa haki kwa kila Mtanzania kuishi katika mazingira safi na salama, lakini pia imetoa wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama na imempa wajibu wa kutoa taarifa anapoona kuna uharibifu wowote. Hivyo tunatoa wito kwa kila mmoja kuiga mfano huu," alisema Mboneke.

Katika tukio hilo, NEMC ilimkabidhi cheti maalumu cha shukrani Mwananchi wa Mkoa wa Tanga, Mohamed Hilal, kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha na kushiriki katika shughuli mbalimbali za utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Mustafa Seleboss, alisema Halmashauri hiyo iko tayari kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa, ikiwamo kuondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga waliopanga biashara zao katikati ya stendi ya daladala.

Aliseam zoezi huilo wamelipokea huku wakihaidi kuendelea kulienzi Jina lake kwa kuhakikisha kila tarehe moja ya kila mwezi wanafanya usafi maalumu na kuanzia sasa wataviondoa vibanda vyote ambapo vimekuwa vimekuwa na uchafu mwingi.

0 Comments