MASHINDANO Ya Urembo Miss Dar zone yachukua sura mpya baada ya kuita Warembo 12 tu kutoka katika mashindano ya wilaya za Dar es Salaam .
Akizungumza na Michuzi Muandaaji wa shindano la Miss Dar zone Ruth Urio Maarufu Kama Mama J'adore amesema kutokana na uzoefu wake wakuandaa mashindano mbalimbali huku akijinasibu kuwa warembo wengi wamepita katika mikono yake huku akitoa Miss Tanzania ambae amefanya vizuri hadi kufikia Miss World Sylvia buberwa ,hivyo kuhaidi kupitia mashindano hayo ya Miss Darzone wategemee Miss Tanzania atapatikana kutoka hapo.
"Mwaka huu tunatarajia kuwa na msimu mkubwa zaidi, wenye ushindani, burudani
na matukio mbalimbali yatakayotufikisha kwenye kilele cha safari hii ya Miss Darzone ambapo tutachukua Warembo 12 tu katika mashindano madogo ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo kwa sasa tunasubiri mchakato wa kupatiwa kwao."
Muandaaji huyo ameongeza kuwa warembo wataingia kambini mwezi Oktoba huku kilele chake Novemba 12,2026 ambapo zawadi kwa atakaevikwa taji ataondoka na gari mpya ambayo itawekwa wazi hivi karibuni aina ya gari hiyo na thamani yake.
Pia amewaomba Wazazi na Walezi kuwaruhusu mabinti zao kushiriki mashindano hayo ya Urembo kwani Urembo sio uhuni kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu badala yake Mashindano hayo yamekuwa yakitoa Wasichana ambao wamekuwa mfano wa kuigwa ,Viongozi wa Kitaifa na Wasaidizi wa Jamii zao.


0 Comments