
Mtangazaji wa Global TV Online, Imelda Mtema, ametoa wito kwa Watanzania na watu wenye moyo wa kujitolea kumsaidia mtoto Malaika anayesumbuliwa na matatizo ya moyo na anayehitaji matibabu nje ya nchi yanayokadiriwa kugharimu Shilingi milioni 70.
Imelda amesema amemtembelea mtoto huyo na kushindwa kuvumilia hali anayopitia, akieleza kuwa mtoto huyo anakabiliwa na changamoto ya kupungukiwa na oksijeni mara kwa mara, hali inayosababisha kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Kwa mujibu wa Imelda, mtoto huyo ana matundu matatu kwenye moyo na anahitaji matibabu maalumu nje ya nchi ili kupata nafasi ya kuendelea kuishi katika hali bora ya afya.
Kupitia ujumbe wake wa kuomba msaada, Imelda amewahimiza Watanzania kuchangia kiasi chochote cha fedha kupitia namba ya simu ya mama wa mtoto huyo, Beatrice Gabriel, 0750 000 930, ili kusaidia kufanikisha matibabu hayo.
Aidha, mtangazaji huyo ameeleza kuwa mama wa mtoto huyo amekuwa akipitia msongo mkubwa wa mawazo kutokana na hali ya kiafya ya mtoto wake na gharama kubwa za matibabu zinazohitajika.
Imelda amesisitiza umuhimu wa jamii kuungana katika kipindi hiki kigumu, akitoa wito kwa watu wenye uwezo na wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia kuokoa maisha ya mtoto Malaika.
Kwa wanaotaka kumsaidia mtoto Malaika, michango inaweza kutumwa kupitia namba ya simu ya mama yake, Beatrice Gabriel: 0750 000 930.
BONYEZA HAPA >> KUONA HALI YA MTOTO MALAIKA

0 Comments