Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya ya waasi wa Kihouthi nchini Yemen, umesema umedungua makombora 10 ya balistiki yaliyorushwa na Wahouthi kuelekea kusini mwa Saudi Arabia.

Msemaji wa muungano huo wa kijeshi, Turki al-Maliki, amesema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X kwamba, “makombora 10 ya balistiki yaliyorushwa na kundi la Wahouthi, ambalo ni kundi la kigaidi, kuelekea eneo la kusini yamedunguliwa na kuharibiwa.”

Mamlaka za Saudi Arabia awali zilitangaza kudungua na kuharibu makombora mawili yaliyorushwa na Wahouthi.

Moja lilikuwa kombora la balistiki lililoelekezwa katika mji mkuu, Riyadh, huku jingine likilenga mji wa Khamis Mushait.

Tangazo la kudunguliwa kwa makombora hayo mawili lilitolewa saa chache baada ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Khalid kutangaza kurejelewa kwa shughuli za kawaida za usafiri , kufuatia kusimamishwa kwa safari za ndege kwa wiki mbili, baada ya mashambulizi ya awali ya makombora.