Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Zuhura Yunus, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Bi. Mary Maganga, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, ulioanza leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam. Wengine pichani kutoka kushoto ni Dkt. Sabelo Mbokazi, Mkuu wa Kitengo Cha Kazi, Ajira, na Uhamaji wa Kamisheni ya Umoja Wa Afrika (AU) Mhe. Sheikha Najwa Bint Abdulrahman Al-Thani, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar na Mhe, Mohammed Hassan Al Obaidli kutoka Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC Bureau)

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Zuhura Yunus, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Bi. Mary Maganga, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, ulioanza leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Zuhura Yunus (katikati), kwa niaba ya Katibu Mkuu, Bi. Mary Maganga, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, ulioanza leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam. Wengine pichani kushoto ni Dkt. Sabelo Mbokazi, Mkuu wa Kitengo Cha Kazi, Ajira, na Uhamaji wa Kamisheni ya Umoja Wa Afrika (AU) na Mhe. Sheikha Najwa Bint Abdulrahman Al Thani, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar.
Washiriki wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira Oktoba 5, 2026 jijini Dar es ssalaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar, Mhe. Sheikha Najwa Bint Abdulrahman Al-Thani, Akizungumza Kwenye kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, ulioanza leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam

Mhe, Mohammed Hassan Al Obaidli kutoka Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC Bureau), akizungumza kwenye kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo (Wapili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda,wakiwa katika ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam.

UJUMBE WA TANZANIA KWENYE ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi nchini Qatar, Mhe. Sheikha Najwa Bint Abdulrahman Al-Thani (Kulia), akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Zuhura Yunus, waki wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, leo Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam.
Baadhi Ya Watendaji Wakuu kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano Kwenye kikao cha Makatibu Wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira Oktoba 5, 2026 jijini dar es ssalaam.

  • Tanzania yasisitiza utekelezaji wa vitendo katika uhamaji wa nguvu kazi Afrika na GCC+
  • Asema Tanzania itahakikisha Maslahi ya Wafanyakzi wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi yanalindwa
Na OWM (KAM) – Dar es Salaam.

Serikali ya Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kulinda haki za wafanyakazi na maslahi ya wahamiaji ili kuhakikisha uhamaji wa nguvu kazi kati ya Afrika na nchi za GCC+ unakuwa salama, wenye haki na wenye tija.

Akizungumza leo tarehe 5 Oktoba, 2026 jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Zuhura Yunus ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo katika Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue uliowakutanisha Makatibu wakuu, Watendaji na Wataalamu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) amesema idadi kubwa ya vijana kutoka nchi za Afrika inaendelea kutafuta fursa za ajira katika nchi za nje hususan katika nchi za Ghuba, na kueleza kuwa kuna umuhimu wa kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa usalama na kulinda haki zao.

“Mafanikio ya Doha Dialogue hayapaswi kupimwa kwa ahadi na makubaliano pekee, bali kwa hatua zitakazochukuliwa katika kuimarisha mifumo ya uajiri, maslahi, usalama na afya mahali pa kazi, upatikanaji wa haki, kinga ya jamii na mifumo ya takwimu za uhamaji wa nguvu kazi,” amesema

Kadhalika, amesema Tanzania ipo tayari kushirikiana na Umoja wa Afrika pamoja na nchi za Ghuba, Jordan, Lebanon na washirika wengine katika kujenga mfumo madhubuti wa ushirikiano utakaosaidia kuimarisha uhamaji salama na wenye staha wa nguvu kazi kati ya Afrika na nchi za Ghuba.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi Qatar, Sheikha Najwa bit Abdulrahman Al-Thani, amesema ushirikiano kati ya nchi za Ghuba na Afrika unapaswa kuimarishwa zaidi sambamda na kubadilishana uzoefu katika kujenga mifumo ya pamoja inayotekelezeka na yenye matokeo.

Vilevile, amesema nchi za Ghuba zimepiga hatua katika kuimarisha mafunzo ya ufundi na stadi, hivyo itatumia uzoefu huo kwa kushirikiana na nchi za Afrika katika kuwaandaa vijana wenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.

Naye, Mkuu wa Idara ya Kazi, Ajira na Uhamaji wa Nguvu Kazi katika Tume ya Umoja wa Afrika, Dkt. Sabelo Mbokazi amesema kuongezeka kwa vijana kutoka Afrika, hususan Afrika Mashariki, baadhi ya nchi za Afrika Magharibi na Afrika Kaskazini, wanaokwenda kufanya kazi katika nchi za Ghuba kunaonesha umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya kanda hizo mbili katika kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi wahamiaji.

Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility) unaratibiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) ukiongozwa na kauli mbiu isemayo “Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na endelevu katika ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+).