Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme Khalid mjini Riyadh, Saudi Arabia, umeshambuliwa tena siku chache baada ya waasi wa Houthi wa Yemen kudai kuhusika na mashambulizi mawili ya awali dhidi ya kituo hicho.

Mashirika ya habari ya kimataifa yamesema shughuli katika uwanja huo zilisitishwa kwa muda na watu kuhamishwa baada ya mlipuko mkubwa kusikika Jumamosi. Shahidi aliyenukuliwa na Reuters alisema zaidi ya magari 12 ya wagonjwa yalionekana yakielekea eneo la uwanja wa ndege.

Mamlaka za Saudi Arabia hazijatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo. Hata hivyo, uongozi wa uwanja wa ndege umewataka wasafiri kuthibitisha taarifa za safari zao na mashirika ya ndege kabla ya kuelekea Riyadh.

Tukio hilo limetokea siku moja baada ya mamlaka za Saudi kusema raia watatu, akiwemo rubani, waliuawa katika mashambulizi mawili yaliyodaiwa kufanywa na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran. Watu wengine watatu pia waliripotiwa kuuawa katika mashambulizi dhidi ya viwanja viwili vya ndege vya Saudi Arabia mapema wiki hii.

Mashambulizi hayo yanajiri wakati mapigano yakiongezeka nchini Yemen kati ya vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia na waasi wa Houthi, ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.

Wahouthi wanasema wanailenga Saudi Arabia kutokana na uungaji mkono wake kwa vikosi vya serikali ya Yemen katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea. Mgogoro huo umeongezeka zaidi baada ya waasi hao kuya Shamu