Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Oktoba 7, 2026, amewasili nchini Uingereza, ambako anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Jukwaa la Uwekezaji la Tanzania nchini humo.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu ataongoza ujumbe wa Tanzania katika mikutano na wadau, wawekezaji pamoja na viongozi wa kampuni mbalimbali zinazofanya shughuli katika sekta za madini, benki, teknolojia, usafirishaji na miundombinu.Mikutano hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji, pamoja na kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana nchini Tanzania kwa wawekezaji kutoka Uingereza na maeneo mengine.

.jpeg)


0 Comments