Wasanii wa Nigeria, akiwemo Tems, Burna Boy, Wizkid na Ayra Starr, ni miongoni mwa wasanii wa Afrika walioteuliwa kuwania tuzo za Grammy za mwaka 2027.
Tems amepata jumla ya uteuzi nne, ukiwemo wa Best R&B Solo Performance, ambako atachuana na Beyoncé, pamoja na vipengele vya Global Music Album na African Music Performance.
Burna Boy pia ameteuliwa kupitia ushirikiano wake na Shakira, huku Wizkid na Asake wakipata uteuzi katika vipengele mbalimbali. Ayra Starr naye ni miongoni mwa wasanii wa Nigeria waliotajwa.
Kwa upande mwingine, mwimbaji wa Uingereza Raye ameongoza kwa kupata uteuzi 11, huku RosalÃa wa Uhispania akipata uteuzi tisa kupitia albamu yake Lux. Mwimbaji mkongwe wa Marekani Dolly Parton, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 80, pia ametambuliwa kwa uteuzi tatu.
Tuzo hizo za 69 za Grammy zinatarajiwa kufanyika Februari 7, 2027, jijini Los Angeles, Marekani.

0 Comments