Askali Magereza mwenye namba za usajiri B50004 ndugu Elias Bukwima amejipiga risasi na kufa papo hapo.Marehemu Elias alijifyatulia risasi tatu kichwani kwake kwa kutumia bunduki aina ya Smg yenye namba za usajiri D61220 aliyokuwa nayo siku hiyo ya tukio kazini kwake.habari zaidi.....
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo lililotokea jana majira ya saa saba mchana wakati askari huyo akiwa eneo la lindo kwenye gereza la Butimba jijini Mwanza.

Maiti ya askari huyo imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando huku polisi wakiendelea kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha mauaji hayo.