Wednesday, August 5, 2015

UN:Shambulio la Burundi lichunguzwe

Mbonimpa
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametaka uchunguzi wa kina ufanywe kwa shambulio lililofanywa dhidi ya mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Burundi.
Pierre Claver Mbonimpa alijeruhiwa vibaya baada ya mtu aliyejihami kumpiga risasi usoni na kutoroka kwa pikipiki.
Mwanawe Mbonimpa, Amandine Nasagarare ameambia BBC kuwa babake bado amelazwa hospitalini japo hali yake sasa imeimarishwa.

Redio yafungiwa Sudani kusini

Sudani kusini ni taifa changa zaidi duniani ambalo maendeleo yake yanafifia kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe
Vikosi vya Usalama nchini Sudani Kusini vimefunga kituo cha redio iliyokuwa ikiunga mkono mpango wa kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo.
Mamlaka ya nchi hiyo, imekilazimisha kituo cha radio cha Free Voice South Sudan kinachoungwa mkono na Marekani kutorusha matangazo yake siku ya Jumanne, siku moja tu baada ya kulifungia gazeti la The Citizen.
Wapatanishi wa kimataifa wamewapa rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar mpaka katikati ya mwezi Agosti kusaini makubaliano ya amani.
Kwa upande wake, rais Obama amewatuhumu viongozi hao wawili kwa kile alichokiita kusambaratisha matumaini ya taifa changa zaidi duniani.
Mpaka sasa maelfu ya vijana wameuawa na takriban watu milioni moja na nusu wamekimbia makazi yao tangu mgogoro huo ulipoanza yapata miaka miwili iliyopita.

Tuesday, August 4, 2015

DK. MAGUFULI ACHUKUA FOMU KWA KISHINDO, AIWASILISHA KWA RAIS KIKWETE KUTHIBITISHA

 Mgombea mteule wa Urais kwa tiketi wa CCM, Dk. John Magufuli na Mgombea mwenza Samia Salum leo .
Msafara wa Magufuli ukipita kwenye makutano ya baabara ya Morogoro na Bibi Titi
 Mwananchi akipunga mkono kufuarhia msafara wa Magufuli.
 Wananchi akipunga mkono kufuarhia msafara wa Dk. John Magufuli wakati ukipita kwenye baabara ya Bibi Titi Mohammed, mgombea huyo akienda kuchuua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 Mgombea mteue wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli akiigia Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi huku akisindikizwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
 Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli akisaini fomu maalum, baada ya kuingia Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu za kuomba kugombea urais. Kulia ni Mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan

BALOZI LIBERATA MULAMULA ATINGA NDANI YA STUDIO YA KILIMANJARO

 Balozi Liberata Mulamula akiwasili nje ya jengo lenye studio ya Kilimanjaro tayari kuongea LIVE katika kipindi cha Jukwaa langu kinachorushwa kila siku ya Jumatatu kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku saa za Mashariki za Marekanui. anayemfungulia mlango ni Abdul Malik

 Balozi Liberata Mulamula akiingia ndani ya studio akiwa amesindikizwa Harriet Shangarai (kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa studio hiyo, kulia ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme na Abdul Malik
 Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa studio meneja ambaye pia ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Jukwaa langu, Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani) Kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akifuatilia maelezo hayo.
 Mhe. Liberata Mulamula akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa meneja wa studio Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha jukwaa lako. Kati ni matangazaji maarufu wa Radio ya Times FM na aliyewahi kutangaza  Radio One Bi. Rose Chitalah ambaye pia anamsaidia Mubelwa Bandio katika utangazaji na kuchangia hoja mbalimbali katika kipindi cha Jukwaa langu.
 Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Mubelwa Bandio (kulia) na Rose Chitalah (hayupo pichani ) na wasikilizaji waliokua na shahuku ya kumuuliza maswali.
  Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani ) na Rose Chitalah (kushoto)
 Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akisikiliza mahojiano na kunakili baadhi ya vipengele katika mahojiano hayo.
 Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakiwa katika picha ya pamoja.
 Kutoka kushoto ni Dj Luke Joe, Meneja wa studio ya Kilimanjaro,  Mubelwa Bandio, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakipata picha ya kumbu kumbu na Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marejkani na Canada na sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Kuelekea uchaguzi mkuu, Waislamu nchini waomba amani itawale


AKutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usuluhishi, Umoja wa Wanawazuoni wa Kiislam Tanzania, Sheikh Ally Said Bassaleh, Mwenyekiti wa Wanawazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Suleiman Amran Kilemile na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Mohamed Issa.
BWanahabari wakifuatilia mkutano huo.
C.Mwenyekiti wa Kamati ya Usuluhishi, Umoja wa Wanawazuoni wa Kiislam Tanzania, Sheikh Ally Said Bassaleh akizungumza jambo.
DViongozi hao wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani).
KUELEKA Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu hapa nchini, Umoja wa Wanawazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay-Atul Ulamaa), wamewataka Watanzania kuilinda amani tuliyonayo.

Rais Nkurunziza aomba utulivu Burundi

Nshimirimana
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameomba utulivu baada ya wapiganaji waliovalia magwanda ya kijeshi kumuua mmoja ya majenerali walio na ushawishi mkubwa serikalini.
Katika hotuba kwa taifa muda mchache tu baada ya shambulio hilo,Nkurunziza aliomba utulivu akisema kuwa kisasi kitamaliza kizazi chote.

Kundi la waislamu lahukumiwa miaka 22 jela

Obama
Mahakama moja nchini Ethioipia imelipiga hukumu ya miaka 22 jela kundi moja la waislamu chini ya sheria tata ya kukabiliana na ugaidi.
Washukiwa hao 18 walishtakiwa mwezi uliopita kwa mashtaka ikiwemo lile la ugaidi na njama ya kubuni taifa la kiislamu.

NGOMA AFRICA BAND WAFANYA KWELI MJINI LIGA,NCHINI LATVIA

FFU-Ughaibuni wafanya kweli Liga Summer Festival 2015


Liga,Latvia

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band maarufu kama
FFU ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki Alien juzi wikiendi walifanikiwa kuwadatisha washabiki wa muziki nchini Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga. bendi maarufu  yenye makao yake nchini Ujerumani inayoongozwa na mwanamuziki mahili Ebrahim Makunja aka  Kamanda Ras Makunja,imejizolea umaarufu wa kimataifa kwa kutumia mdundo wake wa"Bongo Dansi" uliochanganywa na rumba la kukata na shoka mdundo huo umefanikiwa kuwazoa na kuwadatisha akili washabiki wengi wa kimataifa.
Ngoma Africa Band kwa sasa wanatamba na single CD yao mpya 'La Mgambo"
yenye mbili za kumuaga rais JK.
unaweza kuwasikiliza at www.reverbnation.com/ngomaafricaband au uungana nao at www.facebook.com/ngomaafricaband


Monday, August 3, 2015

Jeshi la Nigeria lawaokoa watu 180

Nigeria
Jeshi la Nigeria linasema kuwa limewaokoa zaidi ya watu 180, wengi wao wanawake na watoto, kutoka kwa kundi hatari la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram, katika jimbo la Borno.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji moja wa jeshi amesema kuwa kambi kadhaa za waasi hao zilizoko karibu na mji wa Maiduguri zimeharibiwa na kamanda mmoja wa Boko Haram kukamatwa, lakini duru hizo hazijasema ni lini tukio hilo lilifanyika.

Mkutano wa Injili Washington DC [Aug 14 - 16 2015]

Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries linapenda kuwaalika katika siku tatu za mkutano wa uamsho utakaofanyika hapa Washington DC.

Ni kati ya Agosti 14-16 2015
Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya ama Masanja Mkandamizaji alipohudumu kwa waumini wa jiji la Washington DC na vitongoji vyake siku ya Jumapili 07/07/2013 katika kanisa la THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES

SIKILIZA KWA MAKINI WOSIA HUU WA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE

Jokate: Sijafukuzwa nyumbani kwa Ali Kiba

jokate ali kibaJokate Mwegelo ‘Kidoti’ akiwa na Ali Kiba.
Shani ramadhani
Not true! Staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amekanusha vikali madai kwamba hivi karibuni alitimuliwa nyumbani kwa ‘mtu’ wake, Ali Saleh Kiba maeneo ya Kunduchi-Beach, Dar.

Awali ilisemekana kwamba, mama mzazi wa Kiba ndiye aliyemtimua Jokate kwa kigezo kuwa hamkubali kwani mwanaye ana mchumba mwingine ambaye yupo nje ya nchi.
Kabla ya Jokate kukanusha, gazeti hili lilimuuliza Kiba juu ya ishu hiyo ambapo alifunguka: ““Heee! Hizo taarifa ndiyo nazisikia, hakuna kitu kama hicho halafu mimi na Jokate ni marafiki tu.”
Kwa upande wake Jokate alikuja juu kwamba anazushiwa tu na kwamba hajafukuzwa nyumbani kwa Kiba.
“Sijatimuliwa kwa Kiba huo ni uzushi,” alisema Jokate.

WAKRISTO WA ITALIA WAWEZESHA ZAHANATI YA KISASA VIKAWE


IMG_0282
Mkuu wa Masista Waabuduo Damu ya Kristo, Euprasia Julius akimtambulisha mgeni rasmi na meza kuu kwa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe (hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa Maria De Mathias (MDM) Vikawe, Kibaha.
Na Mwandishi wetu, Kibaha
MGANGA Mkuu wa halmashauri ya Mji Kibaha, Dk. Happniness Ndosi amepongeza shirika la masisita wa Waabuduo Damu ya Kristo kwa kufanikisha ujenzi wa zahanati ya kisasa katika kijiji cha Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Mganga huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa zahanati hiyo,pamoja na kuwapongeza amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yote kwa lengo la kuwezesha kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata kituo na kila wilaya kuwa na hospitali.
Aliwapongeza masista hao kwa kuonesha upendo na huruma kama Biblia inavyomsimulia msamaria mwema ambaye alikuta mtu aliyepigwa na majambazi na kumsaidia.
Aliahidi ushirikiano wa serikali katika kufanikisha usajili wa zahanati hiyo na kuendelea kuisaidia hatua kwa hatua hadi inakuwa kituo mpaka watakapofanikisha safari yao ya kuwa hospitali kubwa ya kisasa.
Mganga huyo pamoja na kutoa ahadi hiyo aliwataka wananchi wa Vikawe kutumia huduma hiyo na kwamba zahanati hiyo itakapohitaji msaada wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) wataletewa kuchukua mgonjwa na kumfikisha panapohusika.
Zahanati hiyo ya DA.MA Africa imejengwa kwa ufadhili wa wakristo wa Italia chini ya usimamizi wa Muitalia, Germano Frioni.
Akitoa salamu zake Muitalia huyo amesema kwamba anawashukuru wakazi wa Vikawe kwa kumpa nguvu ya kusonga mbele hasa kwa kutambua kwamba yeye na marafiki zake wamefanyakazi usiku na mchana kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia marafiki wa Afrika.
Alisema atajitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha changamoto za zahanati hiyo zinafanyiwa kazi.
Aliwaomba wananchi wa Tanzania kuendelea kumuombea yeye na wenzake kama Papa Francis anavyoagiza ili malengo ya safari ya kuwapo duniani yafanikiwe.
Alisema kwamba watoto wake Daniel na Marco (kwa sasa wote ni marehemu) ambao ndio kifupi cha zahanati hiyo DA.MA wamemfanya kujitambua na kusaidia wengine katika kuonesha upendo.
Aidha alisema kwamba ataendelea kukumbuka Vikawe kwani alifika mara ya kwanza mwaka 2005 na kuona hali ilivyokuwa ambapo sasa lipo jengo la zahanati hiyo likiwa limekamilika.
Wazo la ujenzi wa zahanati hiyo , lilitolewa na wananchi wa Vikawe kwa Masisita Waabuduo Damu ya Kristo mwaka 2004 wakati wakiwa katika eneo hilo baada ya kununua ekari 40 kwa ajili ya kilimo mwaka 1994.
Alisema pamoja na maombi hayo na wao wenyewe kutambua kwamba kuna mahitaji makubwa ya huduma ya afya japokuwa kuna zahanati ya serikali, hawakuweza kutekeleza maombi ya wanavijiji hadi mwaka 2011 walipofanikiwa kupata ufadhili kutoka Italia na kuanza ujenzi mwaka 2013.
Katika risala yao walisema kwa ushirikiano kati yao na wafadhili hao wamefanikiwa kuwapo kwa zahanati hiyo yenye mahitaji yote ya msingi kwa mujibu wa taratibu za serikali na kuzidi.
Msoma risala alisema kwamba wataendelea kupanua miundombinu mpaka zahanati hiyo ifikie ngazi ya cha afya na baadae hospitali.
Pamoja na ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa masisita hao wameanzisha shule ya awali kuwaandaa wanafunzi wa darasa la kwanza.
Wamesema kwamba wanaamini kwamba wataendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa afya katika kuimarisha huduma za hospitali hiyo.
Zahanati hiyo pamoja na vifaa tiba pia ina raslimali ya visima vya maji ya mvua ujazo zenye ujazo wa lita laki moja na kingine lita 49 elfu, wanatumia umeme wa sola na jenereta .
Walisema kwamba wanachangamoto ya kukosa umeme wa Tanesco, barabara nzuri na nyumba za wafanyakazi.
IMG_0289
Mwenyekiti wa kijiji cha Vikawe, Kibaha, Shabaan Mgini akiwasalimia wageni waalikwa wakati wa utambulisho.
IMG_0301
Sr. Theresia Rogatus akisoma risala katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa DMD iliyopo Vikawe, Kibaha.
IMG_0323
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa -DMD kijiji cha Vikawe, Kibaha. Kutoka kushoto ni Mdau wa Zahanati hiyo, Dr. Zuberi Mzige wa Hospitali ya Mwananyamala,

FILAMU YA AISHA YAZINDULIWA KWA KISHINDO WILAYANI PANGANI


1- moja
Filamu iliyopewa jina la AISHA imezunduliwa rasmi siku ijumaa ya tarehe 31/7/2015 wilayani Pangani chini ya shirika lisilo la kiserikali la UZIKWASA.
Aisha ni filamu ya tatu katika mfululizo wa filamu za UZIKWASA zikiangazia aina mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike. Filamu hizi ni ni sehemu mojawapo tu ya njia za mawasiliano katika kampeni shirikishi-jamii ya mabadiliko ya tabia inayofahamika kama 'BANJA BASI'!, Pangani, Tanga.
Kabla ya filamu ya Aisha iliyozinduliwa kwa kishindo hivi karibuni, shirika la UZIKWASA tayari limeshatengeneza filamu nyenigne mbili ambazo ni FIMBO YA BABA na CHUKUA PIPI, wengi wa waigizaji waliomo ni wasanii wa vijijini.
Pia filamu hizi zinatokana na maisha halisi na utafiti wa kina katika jamii. Kwa nji hii UZIKWASA inahakikisha filamu zake zinaeleweka na zinafanya kazi kama kioo wka jamii. Lengo ni tuone, tuguswe na hatimaye tuchukue hatua ili kuleta mabadiliko.
Filamu ya AISHA inamhusu mwanamke anayeishi mjini na kuamua kurudi kijijini kwao kuhudhuria harusi ya mdogo wake. Wakati anajikumbusha maisha yake ya zamani, na kukutana na familia yake pamoja na marafiki, kunatokea mkasa wenye athari kubwa katika maisha yake.
Watu wangefumbia macho mkasa huo, lakini Aisha anaamua kupambana nao vikali ili kupata haki yake.
Filamu hii inahusu unyanyaa, aibu na wahanga kulaumiwa, na namna gani inazuia wanawake na wasichana kusema wazi. Pia inahusu baadhi ya mamlaka na viongozi kusita kufatilia ukiukaji wa haki za binadamu.
AISHA imeongozwa na mtaalamu maarufu Chande Omar, imetayarishwa kwa ushirikiano na Kijiweni Production, imefadhiliwa na A. Schindler na Swiss Development Cooperation (SDC) na kusimamiwa na shirika la UZIKWASA.
Filamu ya aisha ni kwa heshima ya wanawake wote waliopitia mikasa ya namna hii.
8- nane
Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Regina Chonjo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, nae alipata nafasi ya kutoa hotuba yake.
6- sita
Producer wa filamu ya Aisha Bwana Emil Shivji akizungumza na wananchi waliohudhuria viwanja vya Bomani.
7- saba
Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA Dokta Vera Piroth akitoa hotuba yake ya kipeke ambayo ilikuwa katika mtindo wa hadithi pamoja na maswali, Ilipendeza sana.
2- mbili
Shamra shamra za ngongoti zikikaribisha wageni waalikwa kwenye uwanja wa Bomani wilayani Pangani palipofanyika uzinduzi wa flamu ya Aisha.
3- tatu
Msanii maafuru wa mashairi Ndugu Mabwingo akitoa burudani jukwaani.

MMLIKI WA ST. MATHEW AIHAMISHA MAHAKAMA KWA GHARAMA ZAKE


court_gavel
Na Mwandishi Wetu, Singida
MDAI katika Kesi ya madai ya talaka Magreth Mwangu dhidi ya Mkurugenzi wa Shule ya St. Mathew, Thadei Mtembei amehoji uhalali wa mahakama kufikia kukagua mali zake siku ya Jumamosi bila kupitia mahakama yoyote hapa Singida.
Kesi hiyo ambayo inasikilizwa mahakama ya Mwanzo Kizuiani Mbagala Jijini Dar es Salaam, juzi (Jumamosi) ililazimika kuhamia mkoani Singida baada ya mdaiwa (Thadei Mtembei) kuitaka mahakama kuhamia mkoani Singida kwa gharama zake ili kuhakiki nyumba ambazo alidai alimjengea Mwangu.
Mtembei katika hoja yake ya kuitaka mahakama kuhamia Singida alisema yuko tayari kulipa gharama zote ikiwemo nauli na posho.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Rajab Tamaambele, na wakili wa Mtembei ambaye ni mtoto wa mke mkubwa wa Mtembei (Peter Mtembei), karani na kesi na mtumishi wa mahakama ni miongoni mwa watu waliofika kwa ajili ya ukaguzi na uhakiki wa nyumba hizo.
Hata hivyo hakukuwepo na wazee wa baraza jmbo ambalo mwangu pia alililalamikia. Mwangu alidai kuwa licha ya kuwa hafahamu sheria kutokana na kutokuwa na elimu hata ya Sekondari lakini kitendo cha mahakama kufika Jumamosi kwa ajili ya kufanya uhakiki na ukaguzi haioni kama ni ha haki na pia kulikuwa hakuna afisa ustawi wa jamii.
Alidai hakimu kuongozana na wakili wa kesi hiyo na kuwa pamoja muda wote haoni kama atatendewa haki katika shauri hilo.
“Mimi nahoji ushirikiano huu kama utanitendea haki kwani watu wametoka pamoja Dar es Salaam wameongozana kwenye magari binafsi nafika eneo la tukio nakuta msafara wa hakimu, wakili wa mdaiwa, mwenyekiti wa kitongoji ukiwa umeshafika mbele ya nyumba ambayo walitaka kuanza kuihakiki” alidai.
Alidai hata Mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba, Mahamoud alisema hajapewa taarifa yoyote ya maandishi kwani alishtukizwa na kupelekwa kwenye nyumba hiyo ambayo alisema hafahamu kama ni ya Mwangu.
Pia alihoji uhalali wa mtoto wa Mtembei ambaye ni wakili kusimamia shauri hilo katika mahakama ya Mwanzo huku mara kadhaa akimtolea maneno ya kashfa kama ni mfunga vidonda tu hawezi kujenga nyumba.
Mwangu alisema alishawahi kuiambia mahakama kuwa nyumba zake za Singida alizijenga na aliamua kuziuza kwa ajili ya elimu ya watoto wake ambao walitelekezwa na baba yao lakini cha kushangaza mahakama kwa amri ya Mtembei ikataka kufika Singida kuhakiki nyumba zake.
Hata hivyo mahakama ilikagua nyumba tatu ambapo moja ilikuwa imeshauzwa kwa Sh. Milioni 15 na nyingine iliuzwa ikiwa katika hatua ya msingi.
Baada ya kumalizika kwa uhakiki huo hakimu Tamaambele alimtaka Mwangu kuhakikisha anawasilisha mahakamani nyaraka zote za nyumba na kuwapeleka watoto mahakamani kabla ya kesi hiyo kutolewa hukumu Agosti 25, mwaka huu.

NYIMBO MPYA YA MSANII LINA ''NO STRESS''

Solar yanufaisha wanawake Unguja

Wanawake wa Unguja wajifunza kuwa wataalam katika nyanja ya sayansi
Hali ya uchumi na mfumo wa maisha umeanza kubadilika kwa baadhi ya wakazi wa Matemwe, kaskazini mwa Unguja, nchini Tanzania.
Hii ni baada ya kuanzishwa kwa mradi ujulikanao kama Barefoot Solar ambao unalenga wanawake wenye umri mkubwa ambao wanaopewa mafunzo ya ufundi wa kutengeza taa zinazotumia nishati ya jua na hatimae kuziuza kwa wana kijiji wenzao kwa bei nafuu.
Kuwepo kwa bidhaa hiyo, kumewafanya wakazi hao kuachana na matumizi ya taa zinazotumia mafuta ya taa ambazo, licha ya kuwa na gharama, lakini pia ni hatari kwa maisha ya watu.
Mwakilishi wa maswala ya Wanawake Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,Anna Collins-Falk
"Kwa kweli tunawalenga kina mama wenye umri mkubwa, ambao wanaelimishwa na kupewa mafunzo nchini India. Hawa ni wanawake wa vijijini ambao baadhi yao hawajui kusoma wala kuandika,

Jenerali Nshimirimana auwawa

Watu waliokuwa na bunduki wamemuuwa mkuu wa usalama wa zamani wa Burundi na mshauri mkubwa wa Rais Pierre Nkurunziza.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema Jeneral Adolphe Nshimirimana alikufa pale gari lake liliposhambuliwa katika mji mkuu, Bujumbura.
Umoja wa Ulaya umesema mauaji yake yamezidisha wasiwasi, na kwamba juhudi za upatanishi lazima zianze tena.

MTOTO WA MAMA NTILIE JUMAA AWESO ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA NDANI CCM PANGANI

aweso
Ndugu Jumaa Aweso.
Na Mohammed Hammie, Pangani, Tanga
Mtoto wa mama ntilie mwenye uzao halisi kutoka wilayani Pangani mkoani Tanga, Ndugu Jumaa Aweso (pichani) ameibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa ndani wa chama cha mapinduzi CCM.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katibu wa CCM wilayani Pangani Bi Zaina Mlawa amesema kuwa, katika uchaguzi huo uliowashirikisha wagombea wapatao kumi na moja, Ndugu Aweso amekuwa wa kwanza miongoni mwa wagombea hao.
Uchaguzi huo uliokuwa na ushindani wa aina yake kutokana na kuwepo kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Ndugu Salehe Pamba, uliwashirikisha wapiga kura wapatao 10376 wa chama cha mapunduzi.
Awali wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Bi Zania aliwataja wagombea hao kwa idadi ya kura walizopata na kusema kuwa "Ndugu Wahi Ibrahim amepata kura 87, ndugu Rosemary Luanda amepata kura 89, ndugu Elizabeth Alatanga amepataa kura 158, Halima Kimbau amepata kura 222, Ndugu Mohammed Rished amepata kura 442, Ndugu Ayubu Mswahili amepata kura 565"
Bi Zania ameongeza kwa kusema kuwa "Ndugu Omary Mwidadi amepata kura 587, ndugu Omary Chambega amepata kura 720, ndugu Salehe Pamba amepata kura 1567, ndugu Abdurahmani magati amepata 1956, na ndugu Jumaa Aweso 3983"
Ushindi huo kwa ndugu Jumaa Aweso unampa nafasi ya kuwa mgombea wa kwanza katika kuipeperusha bendera ya chama cha mapinduzi CCM wilayani Pangani endapo kamati kuu ya maamuzi itaridhia.
Mpaka sasa katika jimbo la Pangani kumepatikana wagombea wawili ambao wanaonekana kupendwa sana na wanancho ambao ni Amina Mwidau wa CUF pamoja na JUmaa Aweso wa CCM ambapo kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya siasa, endapo watakutana katika nafasi ya ubunge upinzani utakuwa wa aina yake.

Friday, July 31, 2015

UTOTO RAHA SANA,KWANZA KUDANGANYIKA NI RAHISI SANA ONA HAPO SASA


GARI LA KUBEBEA MAJENEZA LA KIPEKEE LAINGIA NCHINI


IMG_0469
Pichani juu na chini ni muonekano wa Gari maalum la kukodisha kwa ajili ya shughuli za kubebea majeneza katika misiba limeingia nchini.
Kwa wanaohitaji kukodi kwa shughuli za misiba wanaweza kuwasiliana kupitia barua pepe kiwiaadavidson@hotmail.com au simu namba +255 715 213213, +255 713 616606 na +255 784616606
IMG_0459

IMG_0481
Muonekano wa ndani sehemu maalum linapowekwa jeneza.
IMG_0477

MSIMU MPYA WA KANDANDA NDANI YA DSTV KUTIMUA VUMBI WIKI IJAYO.


IMG_0388
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa msimu mpya wa kandanda kwa wateja wa DStv jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
IMG_0397
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na huduma za DStv. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi.
IMG_0422
Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu, akielezea huduma za kuunganishwa kwa wateja wapya wa DStv, ambapo ving'amuzi pamoja na dishi vinapatikana kwa gharama nafuu kabisa ya Sh.99,000/- kwa mawakala wote wa DStv nchini.
IMG_0443
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi ya begi kwa mwandishi wa habari, Joseph Michael baada ya kuchezesha droo kwa waandishi waliohudhuria mkutano huo. Wanaoshuhudia kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
IMG_0454
Furaha Samalu na Barbara Kambogi wakikabidhi zawadi ya begi Super Sport kwa mpiga picha wa ITV, Abdallah Kaniki aliyeibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa na Multichoice Tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kulia Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.