Rais wa Shirikisho la soka duniani-Fifa, Sepp Blatter, amesema kuingia hatua ya fainali kwa timu ya TP Mazembe kutafuta klabu bingwa ya soka duniani, inaonesha namna soka ya Afrika inavyopiga hatua kubwa.
TP Mazembe ambao ni mabingwa wa soka wa Afrika, watamenyana na mabingwa wa soka wa Ulaya, Inter Milan ya Italia leo Jumamosi.
Akizungumza akiwa Abu Dhabi ambapo mashindano hayo yamekuwa yakifanyika, Blatter ameipongeza klabu hiyo ya Afrika .
DUA KWA KILA MWAFRIKA KWA WAAFRIKA WENZETU,MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TP MAZEMBE YA CONGO.