Michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika kwa mchezo wa Kick Boxing 'K-One Afrika' iliyokuwa imepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, imesogezwa mbele na sasa itafanyika Januari mwakani.
Aidha kutokana na kukosekana kwa wadhamini wa kulipiga tafu shindano hilo, nchi shiriki za kigeni zimepungua toka nane hadi kubakia timu tatu tu ambazo ni Kenya, Uganda na Sudan.
Mratibu wa michuano hiyo, Japhet Kaseba, alisema jana kuwa, michuano yao imesogezwa mbele ili kupisha pambano la ngumi za kulipwa kati ya Mada Maugo na Francis Cheka.