Kumetokea milipuko miwili katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm.
Mtu mmoja aliuwawa na wengine wawili wamejeruhiwa.
Idara ya usalama ya Sweden imesema inachunguza miripuko hiyo kujua iwapo ni ya kigaidi au la.
Waziri wa mambo ya nje wa Sweden, Carl Bildt, alisema hayo yalikuwa ni mashambulizi ya kigaidi yaliyofeli, lakini polisi hawakuthibitisha.
Msemaji wa polisi, Anders Thornberg, aliwaelezea waandishi wa habari juu ya barua pepe waliyopelekewa polisi muda mfupi kabla ya miripuko hiyo kutokea.
Barua hiyo ilitaja kuwepo wanajeshi wa Sweden nchini Afghanistan.