Moja ya kichocheo kikubwa kabisa juu ya uvutaji wa sigara kwa vijana wadogo ni wazazi.Wazazi wanachangia kwa kiasi kikubwa sana kuwafundisha watoto jinsi ya kuvuta sigara pale wanapovuta sigara mbele ya watoto zao.Kitu chochote huwavutia watoto wanapoona wakubwa au wazazi wao wakikifanya mbele yao.kwa mfano,mtoto wako akizoea kukuona unapenda sana kula matunda basi ujue nae atafuata nyendo zako,mtoto wako akikuona unapenda sana mambo ya uongouongo basi ujue nae atafuata tabia yako ya uongouongo.
 Huyu ni mmoja wa watu walioathirika na uvutaji wa Sigara,Sigara uweza kukuathiri kwa njia mbalimbali ndani na nje ya mwili wako bila hata ya wewe kujielewa na mpaka ikifikia wewe ujielewe mambo yanakuwa kama jamaa huyo juu pichani.
Ukiangalia vizuri haya mapafu,pafu la kushoto ni pafu la mtu ambaye  anaonekana ni mtu mwenye afya nzuri na si mvutaji wa sigara ila lina ukungu kwa mbali na hii inatokana na kuwa karibu sana na wavutaji wa sigara na matumizi ya vilevi.na pafu la kulia ni pafu la mtu ambaye ameathirika na uvutaji wa Sigara,je ndugu yangu mpenda sigara kwa picha hizi bado ujazinduka?Zinduka ndugu yangu kwani sigara sio nzuri na wala haina faida kabisa kwa maisha yako.
 Na picha hii inakuonyesha jinsi mtu mwenye mapafu mazuri kabisaa na moyo mzuri kabisa kwa kuwa hatumii aina yoyote ya kilevi au uvutaji wa Sigara.
Kuna baadhi ya nchi watoto uanza kuvuta sigara katika umri mdogo sana,Pichani kijana(amerika ya kusini) huyu ambaye anaonyesha jinsi gani kaweza kuimudu sigara mapema kiasi hiki.