Wakati Tanzania inakwenda na zaidi ya watu Millioni 40 na maendeleo yakizidi kuwa magumu siku hadi siku,Huku wenzetu wa Belgium sensa ya mwaka jana inaonyesha wamekaribia watu Millioni 11...Swali linakuja kwanini nchi yenye watu wachache na maendeleo ni makubwa sana na mazuri,siasa isiyokuwa na matatizo yoyote ukilinganisha na nchi zetu za Afrika zenye maendeleo duni na migogoro kila kukicha?Pichani ni moja ya sehemu maaarufu sana kwa utalii Brussels nchini Belgium.
Huu ndio mnara wa Brussels nchini Belgium,Idadi ya Madungu hayo ndio idadi ya Mikoa yote Belgium,ila kwa sasa litaongezeka moja kuashiria kuna mikoa 10.Nchi nzima ya Belgium ina mikoa kumi,Mikoa 5 inazungumza lugha ya Nederlands na mikoa 5 mingine inazungumza lugha ya French,Huu ni muhtasari tu wa nchi ndogoo ya Belgium juu ya hayo Madungu.