Javier Hernandez ama Chicharito, aliyeingia kipindi cha pili, aliiwezesha Manchester United kuilaza West Brom, ambao walikosa mkwaju wa penalti.James Morrison aliisawazishia West Brom kwa mkwaju mkali wa yadi 20 katika kipindi cha kwanza.
Peter Odemwingie akakosa kuipatia Wes Brom bao la pili baada ya kukosa mkwaju wa penalti baada ya mlinzi Rio Ferdinand kumwangusha chini Jerome Thomas.
Matokeo hayo yameipaisha kileleni Manchester United wakiwa na pointi 41.
Nayo Manchester City imeendelea kutoa changamoto kwa vinara wa ligi ya England, Manchester United baada ya kuonesha soka murua dhidi ya Blackpool na kushinda bao 1-0.
Alifunga bao hilo la ushindi lililoimarisha kileleni Manchester United kwa kichwa baada ya kona iliyochongwa na Wayne Rooney kipindi cha pili baada ya Rooney kufunga bao la kwanza, likiwa bao lake la kwanza la ligi tangu mwezi wa Machi mwaka jana wa 2010 tena kwa kichwa.