Inavyosemekana kuwa aliyekuwa Mbunge wa CCM kabla ya Muheshimiwa Sugu bwana Benson Mpesya amefungua kesi ya madai kwa Mh: Joseph Mbilinyi 'Mr Sugu' kwa kile alichosema akutendewa haki kipindi cha kampeni.Akiongea na waandishi wa habari bwana Mpesya alilalamika kwa mambo makuu matatu ambayo anaona hakutendewa haki kipindi cha uchaguzi.mambo hayo ni....
Anadai kuwa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Monica Saile, ambaye wakati wa uchaguzi alikuwa msimamizi wa uchaguzi, alikuwa na maslahi na Chadema kutokana na kuwa miongoni mwa wanachama wa chama hicho cha upinzani waliopendekezwa kugombea ubunge wa viti maalum.
Madai mengine aliyoyatoa Mpesya katika kesi hiyo ni kwamba, wakati wa mchakato wa kampeni, Mbilinyi, alikuwa akitoa maelezo ya uongo kwamba yeye (Mpesya) amejenga shule ya sekondari mkoani Dodoma, hali iliyowafanya wananchi wamuelewe vibaya na hivyo wakashindwa kumchagua.
Sababu ya tatu iliyotolewa na Mpesya ni kwamba Mbunge wa Chadema, wakati wa kampeni alikuwa akieleza maneno ya uongo kuwa yeye (Mpesya) amejenga vilabu vya kuuzia pombe za kienyeji hali iliyomchafulia sifa kwa wapiga kura ambao walimuona kuwa si mpenda maendeleo kwani fedha alizozitumia kujenga vilabu hivyo angeziwekeza katika kujenga hospitali na shule.
Mpesya katika kesi hiyo anatetewa na wakili wa kampuni ya Mkumbe and Company Advocate.